HEADER

Jumatano, 31 Julai 2013

DVD YA UBATIZO ULIOFANYIKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI KWA NABII FLORA ZINAPATIKANA


Katika DVD hii utapa kusikia ujumbe unahusu UBATIZO uliohubiriwa na Nabii Flora Peter siku ya tarehe 20.07.2013 na pia utapata kuona jinsi Nabii Flora akiwabatiza waumini wa kanisa lake siku ya tarehe 22.07.2013.
Unaweza kuwasiliana na Octavian kwa simu +255 716310661 au tembelea www.nabiiflora.blogspot.com
Unaweza kufika katika kanisa hili lililoko Mbezi Salasala, shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni na uliza kanisa la Nabii Flora watakuonyesha. Kama hujui Mbezi Salasala, ukiwa Mwenge panda magari ya Tegeta na shuka katika kituo ulichoelekezwa
DVD hizi zimetengenezwa na RUMAFRICA (shooting, Editing na Cover Design)
Wasiliana nasi kwa simu +255 715 851523 au tembelea www.rumaafricajobs.blogspot.com au www.rumaafrica.blogspot.com


USIPANGE KUKOSA TAMASHA LA UZINDUZI WA ALBAMU YA SHUJAA YA NEEMA GASPA MWEZI WA TISA


APOSTE GIDEON MUTALEMWA ALIYOYAFANYA MAFINGA IRINGA WIKI YA JANA NA KUSABABISHA KUPATA MUALIKO MWINGINE MKOANI HUMO

Mungu bado anazidi kumtumia mtumishi wa Mungu Mtume Gideon Mutalemwa wa anayeabudu katika kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji lililochini ya Nabii Flora hapa jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita alikuwa katika mkoa Iringa eneo la Mafinga kwa kazi ya Mungu katika mkutano wa nje ulioandaliwa na kanisa la Jerusalem Spiritual Transformation lililoko Lumwago Mafinga Iringa mjini siku ya tarehe 24 hadi 28/07/2013.Na sasa ameingia jijini Dar es Salaam kwa kazi ya Mungu.

Siku ya tarehe 8.2013 anategemea kurudi tena katika mkoa wa Iringa ambapo amepata mwaliko na  Mchungaji Ambakisye wa kuhudumu katika kanisa la HOPE FOR ALL NATION CHURCH MAFINGA IRINGA TANZANIA

Mkutano huo ni mkutani wa nje utakaoanza siku ya tarehe 06.08.2013, eneo: Mafinga Mjini uwanja wa kanisa kuanzaia saa9:00 Alasiri – 12: 00 Jioni.

Kumbuka Apostle Gideon ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na pia anafanya kazi ya kuhubiri katika mikutano mbalimbali, Na sasa hivi ameachia albamu yake ya Sambamba na Yesu ambayo ilifanyiwa shooting upya kwa kiwango cha juu sana.

Unaweza kuwasiliana naye kwa simu: +255 719 697252 au tembelea katika blogu yake ya www.apostlegideon.blogspot.com



Apostle Gideon Mutalemwa akihudumu katika kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji la Nabii Flora Peter lililoko Mbezi Salasala jijini Dar es Salaama. Unaweza kutembelea blogu ya kanisa hili www.nabiiflora.blogspot.com au ingia katika facebook yake kwa jina la Nabii Flora Peter.

APOSTLE GIDEON MUTALEMWA AKIWA MKOA WA IRINGA WIKI YA JANA

Mtume Gideon Mutalemwa akiwasha moto Mafinga
 Kwaya ikimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji

Mtume Gideon Mutalemwa akihubiri kabla kuanza kazi ya kumuimbia Mungu
Kwaya ikifnaya kazi ya Mungu wakati wa mkutano

Kazi ya Mungu ikifanywa na Apostle Gideon Mutalemwa
 Wachungaji na Maskofu wakisikiliza Neno na kusoma Neno la Mungu

Haya sasa, mtumishishi wa Mungu akitumika...kurudisha watu kwa Yesu Kristo
Watu full kujiachia kwa Yesu Kristo

Mafinga ikiwashwa moto na Mtumishi wa Mungu Apostle Gideon Mutalemwa.
Watu walkiselebuka na Yesu wakati mtume Gideon akifanya mambo ya Yesu

mzee wa Sambamba na Yesu, Mtume Gideon Mutalemwa akienda sambamba na akina Kamwene na Mapembeleo mjini Mafinga

Kama wewe hupendi kumuimbia Mungu, Mtume Gideon Mutalemwa atamwimbia, kama unavyoona akifanya mambo.

Jumatatu, 15 Julai 2013

UMESIKIA SHUHUDA MOTO MOTO LAKINI HIZI ZA NABII FLORA ZIMEZIDI....

Tunamshukuru sana Mungu kwa matendo amkuu anayofanya katika kanisa hili kwa kupitia mtumishi wake mpakwa mafuta Nabii Flora Peter. Mungu amekuwa akifanya makuu kwa watu wake wanaofika hapa kanisani na kuombewa na Nabii Flora. Nabii Flora amekuwa akiwakilisha shida za watu kwa Yesu Kristo na Yesu amekuwa akijidhihirisha kwa vitendo.



Katika shuhuda za Jumapili ya tarehe 7.7.2013 ambayo ni siku aliyozaliwa nabii Flora utapata kusikia juu:

1. Kupona UKIMWI
2. Mtoto aliyepotea kuppatikana
3.Mtoto aliyekufa akutana na baba yake maeneo ya Tandika Yombo.
4.kaka kuponywa kidonda kilichomsumbua kwa muda mrefu.
5. Watu kupata fedha na kulipa madeni yao
6. Aliyekuwa kichaa na kuvua nguo, sasa amemaliza masomo yake na ana masters.
7. Aliyekuwa hashiki mimba sasa ajifungua mtoto.
8. Aliyekuwa Miss Kanda Mashariki apona UKIMWI
Na shuhuda nyingi utaziapata


Baadhi ya watakaoshuhudia


MAMA  ALIYEKUWA ANATAFUTA MTOTO APATA MIMBA
Bwana Yesu asifiwe; mimi nilikuja hapa nilikuwa na tatizo la kutokushika mimba, nikamweleza Nabii baada ya maombi ya Nabii nikapewa siku 21 nitakuwa ninamimba. Na kweli zilipotimia siku 21 nimeenda kupima nimekutwa nina mimba, namshukuru sana Mungu.



 MISS KANDA YA MASHARIKI-TANZANIA, MARTHA JULIUS APONA UKIMWI
Bwana Yesu asifiwe, mimi naitwa Martha Julius, nilikuwa miss kanda mashariki (mkoa wa Morogoro, mkoa wa Pwani, na mkoa wa Dar es Salaam) 2004/005 na nilikuwa mshindi namba moja, na hii ilinisababishia kuingia katika mashindano ya miss Tanzania 2004/2005. Mimi kabla sijaja hapa kwa Nabii Flora niligundulika mwaka 2010 kuwa nina HIV. Baada ya hapo nikaanza kuhangaika kutafuta tiba. Niliposikia Loliondo kuna uponyaji nilienda bila ya mafanikio,  baadae nikasikia kuna mtoto anaitwa Subira yuko Masasi na huyo mtoto ni wa miaka 8 au 9 anaponyesha magonjwa yote. Ukishuka Masasi kumfikia huyo mtoto lazima ulipie pikipiki shilingi 20,000. Nilienda kwa yule mtoto na nikakaa wiki mbili nikitumia dawa zake, lakini sikuweza kupona.Ikabidi nirudi hapa Dar es Salaama na nikajiunga na kanisa ambalo sitaweza kutaja jina, nikahudhuria maombi lakini sikupata uponyaji. Siku moja nikaona habari za nabii Flora katika mtandao, ninakaamua kuja hapa kwa nabii Flora.


Jamini nimehangaika sana, na nimepoteza fedha nyingi sana, kwa maana kila unapokwenda kutafuta dawa za kuponya UKIMWI lazima uende na shilingi 500,000. Kwa mfano Loliondo tulienda na shilingi 300,000 kwa mtu mmoja, Mtwara nimeenda mara mbili na shilingi 300,000 na nilitakiwa kukaa huko kwa muda wa wiki mbili  na nijitegemee malazi na kila kitu. Kuna watu wengine wapo hapa dar es Salaam kama watu au watano ambao nao nimekuwa nikiwaendea na sikuweza kupata mafanikio.


Ninapenda kumshukuru Mungu wa madhabahu hii, nilipokuja ilikuwa ni siku ya Jumapili asubuhi na nilionana na nabii Flora nikamweleza kuwa mimi ninaumwa HIV, na nabii akanitabiria kuwa nitapona na nihudhurie siku 21, kweli nikaudhuria siku 21 na siku ya Ijumaa iliyopita ndio nilitimiza siku 21. Nikaja kwa Nabii Flora na nabii akaniambie niende nikapime kama nimepona au sijapona. Nikamwambia nabii ninaomba niongezee siku 7 za ziada, lakini nabii akanambia nimekuambia nenda ukapime na majibu yawe mabaya au mazuri ninaomba wewe uniletee.

Mchungaji Jury akisoma cheti cha Elizabeth Julius kinachoonyesha hana HIV

Ninamshukuru sana nabii Flora kwani tangia nimefika mahali hapa na kupokea uponyaji, sikuweza kutozwa kitu chochote. Ninamshukuru sana nabii Flora kwani nilipofika hapa na kumueleza shida yangu alinisihi sana kuhudhuria maombi, na akasema, siku nikikosa nauli yeye atanipa nauli. Nabii amekuwa akinipa nauli na ikiiisha naenda kwake na ananisaidia 10,000/=. Pia rafiki zangu kama Jack na Catherine wamekuwa wakinisaidia nauli sana, na mapaka nimemaliza siku zanggu 21 na maombi.
Kwa kweli nikuwa na hofu sana kwenda kupima ikapidi niwachukue marafiki zangu Jack na Catherine ili wanisindikize.

Rafiki zake walikuwa na haya ya kusema juu ya Martha Julius:

Jack (kulia) akishuhudia juu ya rafiki yake Miss Kanda Mashariki 2004/2005,Martha Julius alipona UKIMWI

Jack: Bwana asifiwe, kwa jina ninaitwa Jack, rafiki yake na Martha, na Catherine, tuliamua kwenda St. Mary Kawe kupima, lakini Martha akawa anakata kwani alikuwa haamini kuwa amepona. Tulipofika pale akachukuliwa damu na tukasubiri dakika 15, baada ya dakika 15 akaitwa na alipoitwa daktari akampa majibu na kumwambia sasa uko NEGATIVE. Ilikuwa ngumu sana kwa Martha kuamini. Kabla ya kupima, tukiwa kanisani katika maombi tulikuwa tukimwambia achilia moyo wako kwa Mungu na Mungu wa nabii Flora atafanya miujiza, naye alifanya hivyo na kweli amepkea na sasa ni mzima.


APONA UKIMWI BAADA YA KUAMINI KUWA KWA KUPITIA MTUMISHI WA MUNGU NABII FLORA ATAPONA
Bwana Yesu asifiwe, Ninamshukuru Mungu kwani amenitendea makuu katika madhabahu hii. Nilianza kuja hapa mwezi uliopita (Juni) mwanzoni nikiwa na HIV POSITIVE. Kabla ya kuja hapa kanisani kwa nabii Flora baada ya kungundulika nina POSITIVE, nilikuwa s0ina amani, nilikuwa sipati usingizi mzuri, saa tano usiku uzingizi unakuwa umekwisha.

Nilikuja baadaye kukumbuka kuwa kuna mtumishi wa Mungu anaitwa Nabii Flora na kabla ya kuhamia Mbezi Salasala alikuwa Maguruwe. Kipindi hicho cha nyuma kabla sijawa na HIV niilikuwa siamini kuwa Nabii Flora anaweza kutibu UKIMWI, lakini yaliponikuta ikabidi niamini.

Nilikuja hapa kanisani na kuonana na nabii Flora na kumueleza matatizo yangu, naye aliniambia nihudhurie Jumapili nne. Nikajaa Jumapili ya kwanza na ya pili na  wiki ya kukaribia Jumapili yan tatu, siku ya Jumatano nikaja. Nikamweleza Nabii Flora kuwa nimekuja na tatizo langu la HIV lile la HIV, na pia nina malaria na Typhoid. Nabii akanambia nenda Jumamosi ukapime. Ninkamwambia Nabii bado sijafikisha mwezi mmoja kama ulivyosema kwaza nina wiki mbili. Nabii akanambia wewe nenda kapime na jibu utakalo likuta njoo nalo, na jibu likwa Negative au Positive wewe njoo mimi nitajua nikutibu vipi. Siku ya Jumamosi nikaenda hospitali ya kwanza Mwananyamala nikakuta Neagative, nikawa siamini, nika mwambia daktari kuwa kuna majibu umeficha na sio hayo, daktari akanambia yeye yuko kazini kwahiyo ahawezi kudanganya.

Nikaenda hospitali ya pili Kijitonyama, na nilipofika nikaambiwa Negative. Nikampigia simu Nabii Flora. Nimepokea muujiza wangu kabla ya siku 21 hazijafika. Ninamshukuru sana Mungu wa Nabii Flora Peter.

Nabii Flora alikuwa na haya ya kusema: Alipokuja kijana huyu siku ya Jumatano ya wiki ya tatu. Mungu akwa amekuja usiku akanambia ninakuletea watu machoni pako, na aliponiletea watu hawa, nikamuona huyu kijana. Siku ya Jumatano ilipofika nikamwambia Nenda ukapime na umeshapona.


BABA ALIYEKUWA NA KIDONDA KISICHOPONA SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina naitwa Joseph; mimi nilikuja hapa  nilikuwa na kidonda kisichopona kwa muda mrefu, nimezunguka sana bila mafanikio lakini baada ya maombi ya Nabii Flora sasa nimepona, namshukuru sana Mungu wa mahali hapa.




BINTI ALIYEKUWA ANAUMWA NA MENO SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Tumaini; mimi nilikuja hapa nilikuwa na tatizo la meno, meno yalikuwa yaniuma sana hata nashindwa kutafuna andazi, lakini baada ya kuleta dawa ya meno hapa Nabii akaiombea sasa nimepona na ninakula kila kitu. Namshukuru sana Mungu.



MTOTO ALIYEKUWA ANAUMWA SASA AMEPONA BAADA YA KUNYWA MAJI
Bwana Yesu asifiwe; kunamtoto wa mwenye nyumba wetu alikuwa anaumwa sana, sasa mimi kunamaji  ambayo Nabii alikuwa ameyaombea hapa Kanisana, baada ya kumpelekea akanywa Yule mtoto akanyanyuka na akaanza kuongea wakati alikuwa hawezi  hata kuongea.


MTOTO ALIYEKUWA AMEPOTEA SASA AMEPATIKANA
Bwana Yesu asifiwe; mimi nimekuja kutoa shuhuda hapa mtoto wangu alikuwa amepote, lakini baada ya kuja madhabahu hii na kuombewa sasa mwanangu nimempata  kama Nabii alivyonitabiria kuwa mwangu yupo na nitampata, namshukuru sana Mungu.



MTOTO ALIYEPOTEA SASA AMEPATIKANA
Bwana Yesu asifiwe; mimi mwanangu alikuwa amepotea kwa muda wa wiki tatu, lakini baada ya kufika mahali hapa na kuombewa mwanangu nimempata kama Nabii alivyonitabiria. Na pia wakati tunarudi nyumbani mtoto huyu alisimama katikati ya barabara wakati kuna roli kubwa lilikuwa linakuja kwa mwendo wa kasi akasema boranife kuliko kuendelea kuishi, lakini kwa nguvu za Mungu lile gari liliweza kuchuna breki. Namshukuru sana Mungu kwa muujiz wake.




MSANII WA BONGO MOVIE  ALIYEKUWA APATI KAZI SASA AMEPATA
Bwana Yesu asifiwe; mimi ni msanii wa bongo move, nilikuja hapa nikamweleza Nabii kuwa toka mwaka umeanza sijaitwa nikafanye kazi, lakini baada ya maombi ya Nabii juzi nikapigiwa simu na msanii mwenza ananiita nikafanye kazi. Kwa kweli namshukuru Mungu pia nimechaguliwa kuwa kiongozi wa kile kikundi.



MAMA ALIYEZURUMIWA NYUMBA SASA IMERUDI
Bwana Yesu asifiwe; mimi nilikuwa na matatizo katika ndoa yangu lakini, mume wangu alinifukuza tukiwa na nyumba mbili na akaoa mwanamke mwingine lakini baada ya kuja hapa kwa Nabii Flora na kuombewa juzi mwanaume ananipigia simu ananiambia nikachukue nyumba yangu inamtesa. Nabii aliniambia kuwa hawatalala mpaka wamerudisha haki yako. Na kabla ya kesi kuisha wamerudisha nyumba. Namshukuru sana Mungu.
DADA ALIYEKUWA HAPATI WATEJA WA I MAZIWA SASA ANAUZA SI KAWAIDA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina naitwa Angle; mimi nina biashara yangu ya maziwa lakini kwa siku nilikuwa nauza nusu lita au siuzi kabisa, lakini baada ya kuja hapa kwa Nabii Flora na kuombewa  nimepata tenda na  nauza lita 30 hadi 50. Namshukuru sana Mungu.

MAMA ALIYEKUWA ANAUMWA NA KIFUA SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Hawa; mimi ni muhumini mahali hapa, juzi siku ya ijumaa nilikuwa naumwa na kifua kilikuwa kimenibana sana na ninashindwa kuhema, nikamuomba Nabii Flora naye akaniombea kwa muda wa dakika chache, baada 8ya kuombewa nilijisikia wepesi, kifua kilichokuwa kimenibana kikaachia na mafua yakaachia. Kifua change kuuma kilianza siku nyingi tangia mwaka 1997, nimetibiwa Kiroboto nikaambiwa nina pumu, nikachekiwa Muhimbili nikaambiwa  nikaambiwa nina pumu. Juzi nilipokuwa nikienda Moshi barabra ilikuwa chafu sana. Pumu yangu ilikuwa ikianza lazima nikachome sindano za mshipa lakini baada ya kuombewa sasa  ni mzima na sijachoma tena zile sindano  na ninaendelea vizuri kabisa.Ninamshukuru sana Mungu.


MTOTO ALIYEKUWA  ANAUMWA ALMONIA  SASA AMEPONA
Bwana Yesu asifiwe; nilikuja hapa mwanangu alikuwa anaumwa na Almonia kila siku, uso wake ulikuwa umevimba na akawa amebadirika uso wake na kuwa mweupe, lakini baada ya kuombewa na Nabii Flora namshukuru Mungu mwangu amepona na mpaka sasa anaendelea vizuri, Mungu ambariki sana mtumishi wake Nabii Flora.



DADA ALIYEKUWA APEWI PESA YA MATUMIZI NA MUME WAKE SASA ANAPEWA
Bwana Yesu asifiwe; mimi baba watoto wangu alikuwa amenitelekeza anipi matumizi ya watoto, lakini baada ya kuombewa na Nabii Flora sasa anatoa matumizi na nyumbani analala maana alikuwa halali nyumbani, namshukuru sana Mungu.


KAKA ALIYEKUWA ANAUMWA SASA AMEPONA, NA ALIKUWA NA MADENI SASA ADAIWI TENA
Bwana Yesu asifiwe; Kwa jina naitwa Emalus Justin, ninaishi Kunduchi Mtongani, ni mzaliwa wa Bukoba,   mimi nilikuwa nasumbuliwa na Malaria sana, nimekunywa sana vidonge bila mafanikio, nimeenda katika hospitali nyingi kama Mwananyamala,  nimemeza dawa  sana lakini bado nilikuwa naumwa lakini baada ya kufika mahali hapa na kuombewa sasa nimepona. Na pia nilikuwa na madeni sana, nilikuwa na deni lililofikia 500,000/=, nilikua naogopa sana nikidhania nitafungwa.  Nilikaja kwa Nabii Flora na yeye aliniuliza unadaiwa Shilingi ngapi na mimi nilimtaji kiasi nadaiwa,  Nabii akaniambia nakwenda kufunga hilo pepo la madeni na sasa namshukuru Mungu sidaiwi  tena nimeshamaliza madeni yote.


DADA ALIYEKUWA HAPATI MIMBA SASA AMEZAA MTOTO WA KIKE
Bwana Yesu asifiwe
; mimi nilikuja hapa mwezi wa tisa mwaka jana 2012, nilikuwa na tatizo la kutokupata mtoto, lakini baada ya maombi ya Nabii Flora nikapewa siku 14 nitabeba mimba na kweli nilibeba mimba na sasa nimejifungua mtoto wa kike ndo huyu hapa. Namshukuru sana  Mungu.

KIJANA APONYWA NA KIFAFA, UKILEMA WA MGUU NA MKONO WATOWEKA
Bwana Yesu asifiwe;  Kwa jina ninaitwa Maiko natokea Goba hapa Dar es Salaam, nilikuja siku ya alhamisi wiki iliyopita kwa nabii Flora Peter ili niombewe, nilikuwa na tatizo la kuanguka kifafa, moyo wangu ulikuwa unapanda sana, tatizo linguine nilikuwa na mguu mmoja mfupi  na mkono mmoja mfupi  na mwingine mrefu. Nilikuwa kilema toka kuzaliwa kwangu . Ninamshukuru sana Mungu kwani zamani mwezi ukiisha naanguka kifafa, lakini nilipoombewa sijaanguka tena, namshukuru sana Mungu na Mungu azidi kumlinda mtumishi wake Nabii Flora.



Huyu ni dada aliyeshuhudia huyu kijana akisumbuliwa na kifafa na tatizo lake la ukilema.

MTOTO ALIYEKUWA AMEKUFA MIAKA MI TATU APISHA NA BABA YAKE MAENEO YA TANDIKA YOMBO
Bwana Yesu asifiwe; Kwajina ninaitwa M. Martin Meza, ninaishi Goba jijini Dar es Salaam. Nilifiwa na mwanangu tarehe 12.01.2011, nikamzika Goba. Nikaja kumuona Nabii Flora nah ii baada ya kusikia mafundisho yake. Nikaleta picha hapa kwa Nabii Flora na kuiombea akaniambia mwangu yupo na anapatikana Manzese na saa nyingine  Temeke. Nikaenda Manzese na kuuliza watu wa pale wakanambia ni kweli huyu huwa tunamuona hapa Manzese kuanzia saa 3 usiku na 11 alfajiri. Sikumuona Manzese bali nikaacha tu maagizo, na baadae nikaenda Temeke, na nilipouliza wakazi wa pale Temeke wakasema huwa wanamuona majira ya mchana kuanzisa saa 8 mpaka saa 10, anatoka upande wa mmoja na kwenda upande wa pili na akielekea huko harudi, na akirudi anarudi siku ya pili katika muda huo wa saa 8 na saa 10. Nilihangaika kwa wiki nzima bila ya kumpata, na baadae nikarudi kwa Nabii Flora. Nabii Flora sasa huyu mwanao anapatikana Ubungo, na pia anapatiaka Tandika Yombo. Nikaenda Ubungo na nikazunguka sana, na baadae nikakutana na kijana ambaye sikumfahamu akanisalimia shikamoo baba mara tatu na mimi  nikampita..Baada ya hapo nikaenda Tandika Yombo, nikazunguka kule sana, nikampigia simu Nabii Flora na sikupata bahati ya kuzungumza naye, basi nikarudi na kumfuata Nabii Flora hapa kanisani. Nabii akaniuliza ya kuwa kuna kijana mmoja ulikutana naye na akakusalimia, na alikuwa na nguo Fulani, sasa Yule alikuwa ndiye mtoto wako!  Sasa kutokana na kutomtambua, nimemrudishia jukumu Nabii Flora anisaidie yeye.



DADA ALIYEKUWA KICHAA SASA AMEPONA NA KUMALIZA MASOMO YAKE (MASTERS)
Bwana Yesu asifiwe; Kwa jina ninaitwa Mrs. Kaijage, ninamskukuru sana Mungu kwa sababu tangu nimeombewa na nabii Flora mwaka juzi mpaka leo ninaishi kwa amani. Niliugua sana, niliteseka sana, lakini tangia nilipofiika kwa nabii Flora na kuniwekea mkono. Mimi kipindi cha nyuma nilikuwa nimechanganyikiwa na kuwa kichaa, nilikuwa nikiambiwa niinue mikono juu ili niombewe, ninaanza kuvua nguo zangu . Nabii Flora alinipa siku 21 za kupokea uponyaji wangu, na sasa nimepona. Pia nilikuwa na tatizo la kupata mtoto, nabii Flora aliniombea na kuniambia nitapata mtoto tena wa kiume, na ni kweli nimepata mtoto wa kiume. Mwaka jana 2012 nilimwambia Nabii Flora kuwa ninaenda kusoma Masters, na Ijumaa nimemaliza masomo yangu na kufanya mtihani wangu wa mwisho, na leo ninatoa shukrani yangu kwa kuniwezesha kumaliza masomo yangu salama.
Kushoto ni mwanae aliyempata baada ya kuombewa na Nabii Flora

Mpiga Picha wetu Rumafrica
www.rumaafrica.blogspot.com

Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com
kwa maelezo zaidi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...