HEADER

Jumamosi, 29 Juni 2013

RULEA SANGA AFIWA NA MTOTO WA SHEMEJI YAKE EDNARA SANGA MAKONGO JUU DAR ES SALAAM


Rulea Sanga wa Rumafrica
Siku ya jana ilikuwa ni siku yake ya mwisho ya kuishi na sisi Marehemu Vailet Kipangula. Mungu alimpenda zaidi na kuamua kumchukua mida ya saa nane mchana akiwa anaelekea Muhimbili. Vailet Kipangula alikuwa akisumbuliwa na uvimbe tumbo kwa muda mrefu. Marehemu alikuwa akilalamika sana na ikafikiwa wakati akawa anatamani kuchukua kisu kujiua kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.


Marehemu mara ya kwanza alilazwa Muhimbili na baadae kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa matibabu. Alipofika nyumbani hakuweza kumaliza hata mwezi bali Mungu alimuwezesha kutimiza wiki mbili na siku ya jana ya tarehe 28/06/2013 ikawa ndio siku yake ya mwisho.

TARATIBU ZA MAZISHI
Marehemu Vailet Kipangula  atazikwa siku ya Jumapili katika makaburi ya Sinza. Kutakuwa na misa na kumuaga nyumbani kwake Makongo Juu karibu na minara ya ITV kuanzia saa 6:00 mchana - 8 mchana na baada ya hapo kutakuwa na chakula, mazishi yatafanyika saa 9:00 mchana Sinza hapa jijini Dar es Salaam.

Ninawashukuru Wote
Rulea Sanga
+255 715 851523
www.rumaafrica.blogspot.com

Ijumaa, 28 Juni 2013

TAG-TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD WAWEKA WAKFU SHULE YA UPANDAJI MAKANISA NJOMBE



Ikiwa Jopo la Maaskofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God wakiwa wamekutana Mkoani Wilaya ya Njombe kwa ajili ya Kikao Chao Cha Kawaida. Askofu Mkuu wa Kanisa hili Dr. Barnabas Mtokambali ameweka wakfu Shule Maalum Ya Upandaji Makanisa iliyojengwa katika wilaya hiyo imekabidhiwa rasmi kwa Askofu wa Jimbo hilo Mchungaji. Luhwago.

Ujenzi wa Shule za Upandaji wa Makanisa ni Maalum kwa ajili ua utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kanisa la TAG kuwaaandaa watumishi ndani ya Muda mfupi kwenda kuanzisha makanisa

Uzinduzi huo umefanyika leo wakati wa kuhitimisha Mkutano huo wa Maaskofu kutoka Nchi nzima ya Tanzania.

siku Ya Jumapili Askofu Dr. Mtokambali atakuwa kanisa la VCCT kwa ajili ya Kuweka Wakfu Kanisa hilo.








Picha na habari kwahisani ya Samsasali.blogspot.com

Jumatano, 26 Juni 2013

AFRIKA YA KUSINI YAJIANDAA KWA KIFO CHA MZEE NELSON MANDELA


 
SASA kuna kila dalili kuwa taifa la Afrika Kusini, limeanza kujiandaa kukabiliana na tukio zito la kifo cha Rais wa Kwanza wa Taifa hilo, Nelson Mandela (94), ambaye amelazwa kwa siku 18 hospitalini akisumbuliwa na maradhi ya mapafu. Kauli tofauti kuhusiana na mwenendo wa hali ya afya yake na matukio mbalimbali yasiyokuwa ya kawaida yanayoripotiwa kufanywa na familia yake, ndiyo ambayo yameamsha hisia hizo.
 
Taarifa zilizopatikana jana kutoka nchini Afrika Kusini, zinaeleza kuwa watu muhimu katika familia ya Mandela, walikutana kwa dharura na kufanya mazungumzo ya faragha katika kijiji alichozaliwa cha Qunu.

Wakati wanafamilia hao wakikutana, msafara wa magari ya kundi jingine la wanafamilia, ulitemb

elea eneo la makaburi ya ukoo wa Mandela.
Eneo hilo la makaburi ya ukoo lipo mita chache kutoka yalipo makazi ya mdogo wake, Morris Mandela, mkabala na nyumba ya Mandela iliyoko kijijini Qunu.

Haikufahamika mara moja mazungumzo ya wanafamilia yalihusu jambo gani, lakini baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika Kusini, vililiripoti kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Xhosa, wanafamilia hutembelea eneo la maziko iwapo kuna hisia za mmoja wa wanafamilia kufariki dunia na wakati mwingine kufanya tambiko la kimila.

Waliofika eneo la makaburi ni Winnie Madikizela-Mandela ambaye ni mke wa zamani wa Mandela, Waziri wa Utumishi wa Umma, Lindiwe Sisulu na Kiongozi wa chama cha upinzani cha United Democratic Movement, Bantu Holomisa.

Msafara wao ulifika eneo la makaburi jana asubuhi na kulikuwa na taarifa kuwa mtoto wa kike wa Mandela, Makaziwe Mandela, aliitwa eneo hilo.

Waandishi wa habari walizuiliwa kuvuka geti la eneo la makaburi hayo na waliofika nyumbani kwake Qubu, walipigwa marufuku kusogea karibu na nyumba hiyo.

Wanafamilia walioripotiwa kukutana kijijini Qunu ni Mandla Mandela, Thanduxolo Mandela, Ndaba Mandela na Ndileka Mandela na Chifu Bhovulengwe wa Baraza la AbaThembu.

Kikao hicho kinaeleza kuketi kuanzia saa nne asubuhi, lakini baadhi ya wanafamilia waliotakiwa kukihudhuria walichelewa kwa sababu ya kutopata taarifa mapema.

Familia yake yatoweka hospitali

Taarifa zinaeleza kuwa jana hakuna ndugu wa Mandela aliyeonekana katika hospitali aliyolazwa, isipokuwa timu ya madaktari wake ambayo iliwasili majira ya saa mbili asubuhi.

Kutokuonekana kwa wanafamilia hao hospitalini hapo, kulitafasiriwa kuwa ni kutokana na kikao kilichoitishwa Qunu. Napilisi Mandela, ambaye ni kiongozi wa familia hiyo, alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza kuwa familia ya Mandela inakutana kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu afya ya mzee huyo.

Hata hivyo, Napilisi Mandela, alieleza kikao hicho cha kifamilia kinahusu mambo ya kimila na aliyekabidhiwa jukumu la kukiratibu ni Silumko Mandela.

Obama kutomuona

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Rais wa Marekani, Barack Obama hatamtembelea Mzee Mandela hospitalini alikolazwa mjini Pretoria, kwa sababu hakupangiwa kwenye ratiba yake.

Ratiba ya Obama iliyotangazwa wakati wa ziara yake nchini Afrika ya Kusini, inaonyesha kuwa atatembelea Kisiwa cha Robben ambako Mandela alifungwa wakati wa harakati zake za kupigania uhuru.

Pia atatembelea mji maarufu wa weusi wa Soweto na Chuo Kikuu cha Cape Town, jijini Cape Town.

Daktari wake alonga

Timu ya madaktari wanaomtibu, jana ilitoa taarifa kuwa hali yake haijabadilika.

Rais Zuma awatuliza Waafrika Kusini

Rais Jacob Zuma amelihutubia taifa kwa njia ya televisheni na kueleza kuwa hali ya Mzee Mandela inaridhisha, huku akieleza pia kuwa maendeleo ya afya yake hayafahamiki.

Zuma alisema hawezi kujua kama Mandela yuko kwenye hali mbaya, kwa sababu yeye hajui mtu anayekuwa katika hali hiyo anakuwaje, hivyo wenye nafasi ya kuzungumzia suala hilo ni madaktari wake wanaomtibu.

Katika hotuba yake alisema hali ya Mandela imekuwa ikibadilika badilika kila baada ya saa 24, hivyo ni jambo gumu kujua kinachokuja mbele.

Zuma alimtembelea Mandela Jumapili akiwa ameambatana na Makamu wa Rais wa ANC, Cyril Ramaphosa.

MITUME 7 KUOMBEA AMANI TANZANIA NA KUTABIRI KATIKA MADHABAHU MOJA NDANI YA KANISA LA RGC MIRACLE CENTER TABATA CHANG'OMBE

Tangazo limetengenezwa na Rumafrica +255 851523


ASKOFU KAKOBE AMALIZA ZIARA YAKE TORONTO, CANADA


Wadau, nimekuwa hapa Toronto, Canada kwenye mkutano wa Askofu Kakobe. Maelfu ya watu wa kila rangi na hata waislamu walitokea. Kulikuwa na wahindi, wachina, wakorea, wazungu pamoja na waafrika wengi. Tumeshuhudia miujiza! Jana kijana wa kiChina aliyekuwa kwenye wheelchair aliweza kutembea. Bibi ambaye alikuwa kwenye wheelchair miaka 18 aliweza kutembea, viziw walisikia! Watu waliolewa mapepo! Hapa Toronto, Askofu Kakobe amefanya mengi! Mkuanta huo ulikuwa June 20-23, 2013 Rexall Centre, York University. Kweli Mungu anamtumia Askofu Kakobe!










Askofu Kakobe Jukwaani

Walioamua kuokoka

UPENDO BENSON AOMBA WATUMISHI WA MUNGU WAMSAIDIE KUHUSIA NA UJUMBE WA SIMU ALIOUPATA


Kuna hii msg nimepata kutoka kwa rafiki yangu, naomba watumishi wa Mungu popote mlipo mtusaidie sisi wanawake, tusije tukaenda motoni kwasababu ya kujiremba.. nanukuu " Hello Upendo, Praise God, I check your Facebook wall every time I log in because you encourage me through the Word of GOD, I pray that God may increase your knowledge of HIM and bless you. I have watched testimonies of people who died or were taken to heaven and hell by JESUS and I found out that many women who were saved on earth are in hell because of wigs, weaveon, makeup, earings, Jewelry, trousers, filthy revealing clothes. I also learnt about Deut 22:5, exodus 32:1-6- GOD cursed jewelry. I first had many questions but after watching many testimonies of people from different continents and reading the Bible, I believe. Watch testimonies of heaven and hell of Evangelist Margaret AMure, Linda Ngaujah, Sister Ayo, claire Atongo and others." Tunahitaji mchango wako

Jumanne, 18 Juni 2013

RON KENOLY NA DON MOEN KUMPA TAFU ASKOFU KAKOBE NCHINI CANADA ALHAMIS HII



Mwimbaji nguli wa muziki wa injili duniani Ron Kenoly anatarajiwa kuwa mmoja wa waimbaji watakaoimba katika mkutano mkubwa wa injili wa kimataifa ulioandaliwa na askofu Zachary Kakobe ambao unatarajiwa kuanza alhamisi hii tarehe 20 hadi 23/6/2013 katika uwanja wa Rexall Centre Tennis katika jiji la Toronto nchini Canada.

Waimbaji ambao tayari wametajwa kuimba katika mkutano huo ambao umepewa jina la "Toronto Miracle Healing Crusade"ni pamoja na nguli mwingine Don Moen, kundi la wanandugu Krystaal, Martha Munniz na waimbaji wengineo, mkutano huo utakuwa wa kwanza kufanyika katika uwanja huo wa tennis huku pia askofu Kakobe kupitia huduma yake ya BZKIM inafanya kuwa muhubiri wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika mashariki na kati kufanya mkutano mkubwa sehemu ya wazi kama ilivyo kwa watanzania kushuhudia wahubiri wakubwa wakija kuhubiri nchini.

Wiki iliyopita askofu Kakobe alikaririwa akiwatoa hofu waumini wake kutokana na madai ya kwamba amewatoroka na kuwaambia kwamba anakwenda kutimiza agizo la Mungu kuhubiri Canada katika mkutano mkubwa tena akitumia lugha ya Kiswahili. Kama hukusoma BONYEZA HAPA.

MEXICO SCHOOL OF MINISTRY DR. CERULLO MINISTERED A POWERFUL WORD

From the Mexico School of Ministry Dr. Cerullo ministered a powerful word "There’s an awesome power here in Mexico. God is going to do something for His people in Mexico He have never done before. God will open the windows of heaven on Mexico. God’s people are going to see themselves as they are and not as the devil deceives them to believe!"

Ndani ya chuo cha huduma huko Mexco (Mexico School of Ministry), malefu ya watu wamepokea mpenyo wa Kiroho. Wengi wameshuhudia kwamba mambo yanayondeka hayajawahi kutokea. Hakika Mungu ameamua kuwatembelea watu wake.

Kilichonifurahisha ni pale uwepo wa Mungu ulipoenea kwa kila mtu, kiasi kwamba kila mmoja aliweka mikono yake kwa mwingine, maana katika agano jipya, sote tuliomwamini Yesu Kristo ni Makuahani.

"Uongozi wa Blog hii tunamtakia Mtumishi Cerullo maisha marefu yenye uliznzi wa Mungu, ili aendelee kuihubiri kweli ya Neno la Mungu".

ABOUT DR. MORRIS CERULLO
Dr. Morris Cerullo is a man on the move for God. He is a man whose entire life is dedicated to fulfilling the call of God to take the Gospel of Jesus Christ to every living creature.

With over 60 years of ministry God has used Dr. Cerullo to pioneer overseas ministries & open many countries that have been considered closed to the Gospel.

Dr. Morris Cerullo, was raised in a Jewish Orthodox Orphanage until the age of 14 1/2 when he gave his life to Christ.
Because of his faith, he was punished and eventually left the orphange.
Since his call to the ministry at the age of 15, God has used Morris Cerullo to reach multitudes of people around the world in over half a century of ministry. To realize the impact of what this ministry has done is staggering.

Consider:
* Dr. Cerullo has ministered to innumerable multitudes of people face to face.
* Miracle Crusades in which the lame walk, the blind see, the deaf hear, and the Gospel is preached have reached up to 500,000 people in one service.
* Dr. Cerullo has ministered in scores of countries on six continents in person, via satellite, television, radio and literature.
* Over one million Nationals have been trained in his Schools of Ministry.
* Dr. Cerullo has personally ministered to Presidents, Prime Ministers, and heads of state in many nations.

Ministering alongside Dr. Morris Cerullo for over 57 years has been his wife, Theresa. Theresa Cerullo is an energetic and effective part of the Morris Cerullo World Evangelism ministry, serving as the official Corporate Secretary/Treasurer. She is lovingly referred to as "Mama" by the millions of Nationals around the world.
"Sir, you are a blessing to our generation.
May God's blessings increase abundantly in your life.
We love you".

"WEKEZENI MASHAMBANI" MASANJA MKANDAMIZAJI

Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji
Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji amesema kuwa vijana wanapaswa kufikiria namna ya kuwekeza mashambani kwenye fursa za kutosha kuliko kuendekeza majivuno yasiyo na msingi.

Akizungumza na Starehe Masanja alisema anafurahi kwani mwaka huu amefanikiwa kuvuna tani kadhaa za zao la mpunga katika shamba lake lililopo Mbarali Estate.

“Nimelimia Mbarali Estate namshkuru Mungu kwa kufanikiwa kuvuna mpunga wangu baada ya kuwekeza shamba lenye ukubwa wa ekari 15, huu ni uwekezaji mzuri unaotoa matunda kwa muda mfupi iwapo utahudumia shamba lako ipasavyo.”

“Vijana wengi wana nguvu na uwezo wa kuingia mashambani ila wanaendekeza ‘usharobaro’ kitu ambacho hakina mavuno kwao,” alisema Masanja aliyetumia mashine ya kisasa katika zoezi hilo.

Masanja ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya New Jerusalem alisema: “Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti,” alisisitiza!

Kwa sasa, Masanja anahudhuria ibada katika kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya ‘Hakuna Jipya’ iko mitaani.

Inatoka: Gospel Vision TZ

PASTOR STEVEN WAMBURA, JAMES KALEKWA, FRED MSUNGU NA MC PILIPILI WAFANYIKA BARAKA KWENYE KINGDOM EXPLOITS.

Katika Chuo cha Mt. Agustino-Mwanza, kulikuwa na Event iliyopewa Jina la Kingdom Exploits, iliyoandaliwa maalum kabisa kwa ajili ya Vijana waliopo chuoni hapo. Tukio hili lilianza Mida ya Saa 2:00 Usiku hadi Saa 5:00 Usiku huku Wanenaji wakiwa ni Bw. James Kalekwa-Mwanza, Fred Msungu-Dar na Mch. Steven Wambura-Dar.
Mchekeshaji wa Kimataifa toka Tanzania, Dar es salaam Bw. Emmanuel Mathias a.k.a Mc Pilipili alikuwepo Ukumbini hapo kuvunja mbavu za Wanafunzi wa Chuo hicho. Shughuli ilifanyika katika Ukumbi wa M10, na Praise Team iliyoundwa na Vijana wa Tafes, Casfeta, Huima na Uscf iliuongoza Umati wa Vijana waliokuwepo katika kuusogelea Uso wa Mungu.

Sasa tazama picha hizi uone jinsi Mambo yalivyokuwa chini ya Mc wa Event Bw. Barnabas Shija.

Mc wa Event Bw. Barnabas Shija

Wanafunzi waliohudhuria

Presentation ya Bw. James Kalekwa

Huyu jamaa hata kwenye Uimbaji yuko vizuri. Ni Fred Msungu

Bw. Fred Msungu akihudumu

Wakati wa Panel Discussion

Mc Pilipili akiingia kwenye Jukwaa tayari kufanya mambo yake 

Mc Pilipili baada ya kumaliza Show yake

Bw. James Kalekwa akihudumu katika Uimbaji

Pastor Wambura akiwaombea Wanafunzi wa SAUT

Kutoka Kushoto ni Barnabas Shija, Pastor Wambura na Mc Pilipili

Team Tukio

Kuanzia Kushoto ni Pastor Steven Wambura, Mc Pilipili, James Kalekwa, Billy, Fred Msungu, Adolph Nzwalla na Sowane Emmanuel.

Jumatatu, 17 Juni 2013

NEW DAY FOUNDATION CHINI YA UPENDO KILAHIRO YAFANYA MAAFALI YA KWANZA YA MAFUNZO YA USHONAJI

Siku ya jana ya Jumamosi  kulikuwa na maafali ya kwanza  ya wanafunzi waliokuwa wanahitimu masomo ya ushonaji katika  chuo cha NEW DAY AFRICA FOUNDATION  Tegeta Kibaoni jijini  Dar es salaam. Chuo kipo chini ya Mkurugenzi Bi. Upendo Kilahiro na Bw. Amon Kilahiro.
 Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro

Unaweza kujiuliza Upendo Kilahiro na Amoni Kilahiro ni watu gani? Upendo Kilahiro ni mke wa  Amon Kilahiro wanamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za injili hapa Tanzania. Baada ya kuona haitoshi kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji  tu wakakaa chini na kupiga magoti mbele za Mungu ili awawezeshe kuwapa kitu kingine cha kuisaidia jamii kimwili na kiroho.

Mungu aliweza kujibu maombi yao na kuwapa kibali cha kuwasaidia Watanzania wenye uhitaji wa kujifunza masomo ya ushonaji . Ndipo  walipoamua kuanzisha chuo cha  ushonaji  kilichopo Tegeta Kibaoni mwaka 2013. Maono yao ya kuanzisha shirika la NEW DAY AFRICA FOUNDATION  yalianza mwaka 2011 na utekelezaji ukawa mwaka 2013.
 Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akiwa na baba yake ambaye alikuwa mgawaji wa vyeti siku hii

Mungu ameweza kumpa moyo wa pekee wa huruma na upendo kama jina lake linavyoitwa “UPENDO”. Bi. Upendo na mume wake Amon Kilahiro wamekuwa wakitoa mafundisho hayo ya ushonaji bure na bila ya malipo yoyote. Wanafunzi wamekuwa wakitumia vyerehani vyao bila ya malipo yoyote, gharama za uendeshaji kama umeme unaotumiaka kuendesha mashine za ushonaji zimekuwa zikitolewa  Wakurugenzi hao (Upendo Kilahiro na mume wake). Kwakweli huu ni upendo wa hali ya juu ambao unahitaji kuigwa na watu wote, kwani unaweza kufikiria jinsi maisha ya sasa yalivyoo magumu, lakini watu hawa hawakuweza kuliangalia hilo bali waliangali sana kusaidia wale wenye uhitaji wa kusoma na hawana pesa za kulipia mafundisho yao.
Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akiwa na furaha ya ajabu kutimiza ndoto yake, Vazi alilovaa limebuniwa na wanafunzi wake.
Wahitimu walimshukuru sana Mungu kwa kuwapa mama na baba ambao ni Upendo Kilahiro na mumwe wake Amon Kilahiro kuwafungua katika giza na kuwaweka katika nuru ya mafanikio ya kimaisha. Elimu waliyopata sio elimu ya theory bali ni elimu ya vitendo.

Wahitimu walionekana kuwa na sura za huruma wakati kumuaga Upendo Kilahiro na mwalimu wao  kwani walisema wanatamani kuwa naye siku zote , na hii ni kwasababu ya upendo waliokuwa nao wakati wapo masomoni na wengine walioneka kutokwa na machozi.  

Wahitimu hao waliweza kuimba wimbo wa kumuaga Upendo Kilahiro,  mwalimu wao na uongozi mzima wa chuo hicho. Wimbo ulikuwa umejaa majonzi  kutokana yale waliotendewa wanahitimu hao wakiwa masomo.Walisema wamejifunza mambo mengi ya kimwili na kiroho na kubwa zaidi wamejipatia ujuzi wa ushonaji.
 Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akimshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufika pale alipokuwa akiota kila siku kupafikia.
Kuna baadhi ya wanafunzi waliweza kupita mbele na kueleza kile ambacho wamekipata chuoni. Baadhi yao walisema wao walifika pale chuoni wakiwa hawajui hata kuchomeka sindano katika mashine ya kushonea, ila baada ya kufundishwa na mwalimu wao waliweza kujua kuchomeka sindano na kuweza kushona nguo za aina yoyote. Wahitimu hao walisema kwa sasa wanaweza kushona mshono wowote.

 Hapa ni nyumbani kwa Upendo Kilahiro Tegeta Kibaoni

Mbali ya hayo yote, Mkurugenzi Upendo Kilahiro alimshukuru sana Mungu kwa kutimiza ndoto yake aliyokuwa nayo kwa muda mrefu ya kuweza kusaidia jamii. Kwake anasema ni mmoja wa muujiza mkubwa Mungu amefanya katika maisha yake. Upendo alionekana kuongea kwa hisia kali sana juu ya mafanikio aliyokuwa nayo. Amesema mara nyingi amekuwa busy sana na kazi za kifamili, kihuduma katika kazi ya Mungu, safari mbalimbali nje ya Tanzania kama UK na Canada kwa kazi ya Mungu na
wakati huo huo anatakiwa kutimiza ndoto yake ya kuisadia jamii hasa suala hili la wanafunzi wa ushonaji. Amekuwa akijibana kwa mambo mengi hasa katika suala la pesa ili kuhakikisha hawa wanafunzi wanapata mahitaji yote ya msingi katika suala lao la ushonaji.
 Mpambaji akiwa kazini kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

Wanafunzi waliweza kuvaa sale zao ambazo wamezitengeza wenyewe na liliwemo vazi alilo vaa Upendo Kilahiro. Wanafunzi hawa ukiangalia mavazi hao, kwa kweli utasema ni wabunifu wa hali ya juu sana
 ..mmoja wa viongozi wa juu katika New Day Africa Foundation akiwa na furaha ya ajabu

UPENNDO KILAHIRO alisema anajisikia kuwa mpweke sana kwa kuangana na wanafunzi hawa kwani amekuwa akiishi nao kama familia na sio kama wanafunzi. Ila alisema kila jambo lina mwanzo na mwisho kwahiyo hata hawa wanafunzi wake umefika wakati wa kuondoka. aliwaomba wanafunzi wazidi kufika chuoni hapa kama kuna jambo watakuwa wanahitaji kutoka kwake, milango iko wazi na yeye atawasaidia bila ya kujali kuwa wamemaliza masomo yao.
 Wa pili kutoka kulia na mama na Upendo Kilahilo na anayefuatia ni baba na upendo Kilahilo wakiwa katika picha ya pamoja.


Alisema lengo lake ni kuona hawa viajana wanapata kazi zao za kujitegemea ili waweze kuwa mchango mkubwa katika Taifa la Tanzania kwani bado wana nguvu za kulitumikia Taifa lao. Watu kama hawa ambao walikuwa hawana ujuzi wako wengi sana mitaani wanashindwa watu wa kuwainua ili wasimame wenyewe, alisema.
-------------------------------------

Katika hotuba yake, alikuwa na haya machace ya kusema:

NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)

NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)  ni shirika la Kikristo linatoa huduma za kiroho na za kijamii. Shirika hili lilianza rasmi mwaka 2011 chini ya mbeba maon Bi. Upendo Kilahiro na daadae shirika hili lilipanuka na kuongeza kwa kusaidiwa na mumewe Bw. Amon Kilahiro hadi kupata uongozi wa

NEDAFO.
Shirika hili lilianza hapa Tanzania lakini lina maono ya kusambaa mataifa yote ya Afrika kwa lengo la kuwapa elimu na tumaini jipya kwa kila mmoja hasa wanawake, wasichana na watoto.

Shirika hili lilianza miaka mitatu iliyopita lakini mwaka huu 2013 tumeanza kutoa huduma za kijamii. NEDAFO imeweza kutoa mafunzo ya ushonaji kwa wanawake na wasichana, nah ii ni sehemu tu ya mengi  ambayo NEDAFO inamtumainia Mungu kutuwezesha kuyafanya katika siku za usoni ili kufikia lengo la maono tuliyonayo.

 Wahitimu wa chuo cha NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO) wakiwa katika picha ya pamoja.
Shirika hili limekuwa likiwafundisha wanafunzi bure na Mkurugenzi amekuwa akiwajibika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, vitendea kazi vya kisasa vinakuwepo, ma pia kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika maadili yale Mungu anahitaji kwa kila mwanadamu kuwa nayo.
 Mavazi haya waliyovaa hawa wahitimu yamebuniwa na wao wenyewe.

UTENDAJI
NEDAFO inafanya kazi ya kuwaendeleza wale wenye uhitaji wa kujiendeleza ili waweze kujikimu katika maisha, kujisimamia kujiajiri na kuweza kuwasaidia wengine kwa yale waliojifunza katika shirika hili la NEDAFO

MUNGU AWABARIKI

 Huu ni uongozi wa NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)

Wahitimu wakiwa wamejiaandaa kupokea vyeti vya kuhitimu
 Wahitimu wakionyesha mishono ya mavazi yao waliyoibuni wakiwa chuoni







 Kulia ni mtoto wa Upendo Kilahiro ambaye naye amejifunza kushona nguo kwa kutumia mashine za kisasa zilizopo hapo chuoni. Hapa akionekana akisali wakati wa kuombea chakula na vinjwaji
 Wahitimu wakiwa katika sala ya kuombea vinywaji na chakula

 Mkurungenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION, Upendo Kilahiro akijitambulisha
 Mwalimu wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION akijitambulisha

 Mkurugenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION Upendo Kilahiro akiongea na wahitimu

 Mkurugenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION akiita majina ya wahitimu kuchukua vyeti vyao vya kumaliza mafunzo ya ushonaji.










 Wahitimu wakionysha vyeti vya vya ushindi kumaliza masomo yao ya ushonaji.


 Mwalimu akiwa na wahitimu wakiimba wimbo wa kuagana na uongozi mzima wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION



WASILIANA NA UPENDO KILAHIRO KWA SIMU

+255 757 578114


KAMA UNGEPENDA KUJIUNGA NA CHUO HIKI
Mpiga Picha
Rumafrica
www.rumaafrica.blogspot.com


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...