HEADER

Ijumaa, 12 Julai 2013

NEEMA GASPA KUMILIKI BLOGU YAKE YA KIKRISTO

Neema Gaspa ni mwimbaji wa nyimbo za injili, siku ya Jumatatu ameweza kufungua blogu yake mpya inayoenda kwa link hii: www.neemagaspaa.blogspot.com. Katika blog hii utapata kujua mengi kuhusu yeye na huduma yake.

Neema Gaspa akiwa katika ofisi ya Rumafrica Sinza Afrikasana

Blogu hii itakuwa inaweka habari za Mungu kutoka madhehebu mbalimbali nchini Tanzania na nje ya Tanzania. Lengo kuu ni kumtangaza huyu Yesu Kristo kwa njia ya mitandao.

Blogu hii imetengenezwa na RUMAFRICA. Rumafrica wanajishughulisha a shughuli za Graphics, shooting, kutengeneza blogs, websites, na kupiga still picture. Unaweza kuwasiliana nao kwa simu +255 715 85 15 23 au tembelea www.rumaafrica.blogspot.com au www.rumaafricajobs.blogspot.com


Neema Gaspa kwa sasa anajiandaa na kuzindua albamu yake inayoenda kwa jina la SHUJAA itakayofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza siku ya tarehe 01.09.2013 kuanzia saa 7:00 mchana na kuendelea. Kiingilio ni Tsh. 10,000 kwa VIP, watoto ni Tsh. 2,000 na viti vya kawaida ni Tsh. 5,000.

USIPANGE KUKOSA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA NEEMA GASPA INAYOITWA SHUJAA MAENEO YA UBUNGO PLAZA

Alhamisi, 11 Julai 2013

APOSTLE GIDEON MUTALEMWA KUFANYA HUDUMA MAFINGA MKOA WA IRINGA

Mungu wetu ni Mungu ambaye hutumia watu wake kwa kazi yake. Katika waimbaji wote Mungu ameweza kumuona mtumishi wa Mungu Mtume Gideon Mutalemwa kwenda Iringa katika kanisa la Jerusalem Spiritual Transformation lililoko Lumwago Mafinga Iringa mjini siku ya tarehe 24 hadi 28/07/2013. Mtume Gideon Mutalemwa atakuwepo pale kwaajili ya kumwimbia Mungu na kumtangaza huyu Yesu tunayemtumikia kila siku.


Apostle Gideon Mutalemwa katika kanisa analoabudu la Yesu Kristo Huduma ya Maombezi na Uponyaji DSM

Mtume Gideon Mutalemwa ni muumini wa kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji Mbezi Salasala kwa Nabii Flora hapa jijini Dar es Salaam. Ni Mtumishi mwenye mke mmoja ambaye ni mzawa wa Iringa na mtoto mmoja. Kwahiyo anapokuja huko Mafinga Iringa anakuja nyumbani.


Watu wa Iringa msipange wa kufikiria kukosa kufika Lumwago Mafinga maana Mungu wetu tunayemwamini ataenda kuonekana na kuhudumia miyo yote kwa kupitia karama aliyoweka kwa Mtume Gideon Mutalemwa.


Mungu amemuwezesha mtumishi kuwa na albamu yake inayoenda kwa jina la SAMBAMBA NA YESU na nadi ya albamu hii utweza kusikia na kuona nyimbo za kitamaduni na nyine nyingi zenye ujumbe mzuri wa Mungu.



Unaweza kuwasiliana na Gideo Mutalemwa kwa simu +255 719 697252 au kwa blogu hii www.apostlegideon.blogspot.com
KARIBUNI SANA

Jumatano, 10 Julai 2013

USIKOSE KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA SHUJAA YA NEEMA GASPA-UBUNGO PLAZA

Umehudhuria matamasha mengi lakini hili si la kukosa kwani kuna kitu Mungu anaenda kufanya juu ya maisha yako katika siku hii ya uzinduzi wa albamu ya mwaimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili Tanzani Neema anayeenda kuzindua albamu yake ya kwanza inayoenda kwa jina la SHUJAA. Utakuwa unajiliuliza ni nani Shujaaa..majibu anayo Neema Gaspa.

Neema Gaspa

Mungu anamtumia sana huyu mtumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji.  Neema Gaspa anatumia ujana wake kwa kazi ya Mungu, na huu ni moyo wa kipekee sana. Neema Gaspa baada ya kuona watu wengi wanauhitaji na kiu ya kutaka kufaidika na karama yake ya uimbaji, sasa ameamua kuzindua albamu yake ili karama yake wapate kuisikia na mwisho wa siku ni kumpa Mungu utukufu kwa maana YEYE anastahili.

Tunachokuomba ni wewe kufika katika eneo la tamasha Ubungo Plaza ili kumuunga mkono mtumishi wa Mungu. Umefika wakati wa kuwa busy sana kumtafuta Mungu. Unaposikia jambo fulani linafanyika kwa utukufu wa Mungu unatakiwa kuamka na kukimbia kumsifu Mungu wetu. Naye Mungu atajisikia furaha sana kuona mtoto wake ameacha kazi zake na kuungana na watu wanamsifu.

Sasa usikose kabisa kufika katika uzinduzi huu. Ikiwezekana mtaarifua na rafiki yako ili aweze kupokea muujiza wake kwa njia ya uimbaji.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huu ni Mheshimiwa Samweli Sitta  aliyekuwa Spika wa Bunge katika Jamhuri ya Tanzania
Mh. Samweli Sitta

Uzinduzi utafanyika katika jengo la kifahari la UBUNGO PLAZA, kwani hata MUNGU wetu wa kifahari sana na wa thamani sana ndio maana tumeona lazima asifiwe katika eneo linaloendana  na uthamani wake
Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam

Kutakuwa na waimbaji wengi sana wa kimataifa kutoka nchini, baadhi yao ni kama:

AMBWENE MWASONGWE

BAHATI BUKUKU


EDSON MWASABWITE
 EVELYN MSOMA


MADAM RUTI

MARTH MWAIPAJA

MAXIMILLANI MWANAMAPINDUZI
 ENOCK JONASI

KIINGILIO KITAKUWA KAMA IFUATAVYO


Jumanne, 9 Julai 2013

MTANGAZAJI WA RADIO WAPO FM TANZANIA AVAMIWA, KUPORWA NA KUKATWA KISU KOONI





Katika hali ambayo inaashiria kwamba usalama wa watu na mali zao katika uwanja wa taifa hususan siku za matamasha hautoshi, mtangazaji na fundi mitambo wa WAPO Radio FM, Filemon Rupia, maarufu kama Father Filemon Rupia, amevamiwa usiku wa tamasha la matumaini na watu wasiojulikana, ambapo walimpora vitu kadhaa ikiwemo simu zake, pesa na kisha kumkata na kitu kinachosadikiwa kuwa ni kisu kwenye koo lake.

Tukio hilo linasemekeana kutokea majira ya saa mbili usiku, ambapo Filemon Rupia na wafanyakazi wenzake wakitokea kwenye ibada ya ujazo wa Roho Mtakatifu maeneo ya Mbezi Beach inayofahamika kama Oparesheni Takasika, walifika maeneo ya uwanja wa taifa, ambapo Father Rupia aliamua kurejea nyumbani kutokana na uchovu, ambapo wenzake walimuacha kwenye lango la kuingia uwanjani - ambapo alianza kutafuta usafiri wa kurudi nyumbani kwake.

Laiti kama angejua kilicho mbele yake, hakika angeingia na wenzake uwanjani, lakini mwanadamu ni mwanadamu tu. Kilichotokea wakati akitafuta usafiri ndio hiki tunachozungumza sasa, kuvamiwa, kuporwa, na kukatwa na kisu kwenye koo lake, ambapo haijajulikana lengo hasa la wavamizi hao kufanya hivyo ilikuwa ni nini.

Hata hivyo Mungu ashukuriwe, kwani kwa hivi sasa Filemon Rupia anaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma kwenye hospitali ya Kairuki, amapo alishonwa nyuzi kadhaa kwa ndani na nje ya koo. Tutakufikishia taarifa zaidi pindi ambapo tutazipokea kutoka kwenye vyanzo vyetu. Kwa hivi sasa anahitaji maombi yako kuvuka hali aliyonayo.

Maelezo ya Rupia

Hatimaye baada ya kufanya mawasiliano na Rupia, anaeleza kuwa akiwa anataka kuchukua bodaboda eneo la uwanja wa taifa, ndipo hapo dhahama lilitokea.

Bodaboda mbili zilikataa kwa maelezo kuwa kuna mtu anasubiriwa, bodaboda ya tatu ikadai kuwa haiwezi kwenda mbali. Ndipo hapo akalazimika kusogelea bodaboda za mbele zaidi ili apelekwe nyumbani, kilichofatia hao ni roba ya mbao, na kuvamiwa na vijana kadhaa ambapo katika purukushani, walitoa kisu na kuanza kumkata kooni, ambapo kisu kilikata ubao na kumchana eneo la kidevu na shingo. Na kama sio ubao kuwepo katikati, basi yangekuwa mengine kwa hivi sasa.

Mara baada ya ya hapo, ikafuata kuzirai kwa dakika kadhaa, na alipozinduka, ndio akasogea hadi getini kuomba msaada, ambapo walikwenda hadi kituo cha Polisi kabla ya kuelekea hospitali ya Temeke (ambapo huduma zilikuwa hafifu) na baadae kurudi nyumbani kwa ajili ya kwenda hospitali ya Kairuki.

Wakati haya yote yanatokea, alikuwa akizungumza na mfanyakazi mwenzake, Joyce Mathew, ambaye baada kufuatilia tukio lote kupitia simu kuanzia wanamkaba na hadi kuiba mali zake, aliwasiliana na wakubwa zake, ambapo msaada ulifanikiwa kupatikana kwa wepesi zaidi.

Pamoja na yote haya, hapa ndipo tunakumbushwa kuwa kila mara jua likizama na tukalala na kuamka salama, basi sifa na utukufu tukumbuke kumrejeshea Yesu Kristo anayetawala muda wote.

source:gospelkitaa

Jumatatu, 8 Julai 2013

HAPPY BIRTDAY NABII FLORA PETER KWA KUTIMIZA MIAKA 29 LEO TAREHE 07.07.2013


Jumapili ya leo ilikuwa ni ya kipekee sana kwa waumini wa kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji Mbezi Salasala hapa jijini Dar es Salaam. Nabii Flora amezaliwa siku ya leo akiwa kanisani. Wapo watu wengi wanazaliwa siku ya leo wakiwa katika mabaa na sehemu mbaya, lakini tunamshukuru Mungu kwa kumuwezesha Nabii Flora kuzaliwa siku ya leo akiwa kanisani na watu wa Mungu.

Kwa kweli Mungu ni mwema kwa kumtimizia miaka 29 Nabii Flora Marco. Mungu amekuwa mwema sana katika huduma yake ya kurudisha watu kwa Mungu. Watu wamebarikiwa sana na siku ya leo. Kanisani kulifanyika tamasha kubwa sana kwaajili ya kumpongeza Nabii Flora kutimiza miaka yake 29. Nabii Flora aliwashukuru sana waumini wa kanisa hilo kwani amesema wamefanyika kuwa kama familia yake.

Nabii alionekana kuhuzunika pale tu alipoweza kutoa historia ya maisha yake kabla na baada ya kuwapoteza wazazi wake wote wawili. Historia hii iliwagusa sana watu wengi waliofika na kuhudhuri siku ya kumpongeza Nabii Flora. Ni mengi Nabii Flora amepitia katika huduma yake ikiwa ni pamoja na kupata vipingamizi vingi katika kazi ya Mungu. Alisema ilifika kipindi akawa anakula na kunya maji ya nazi kutokana na kutokuwa na chakula ndani ya nyumba yake.

Nabii Flora alimshukuru sana Mchungaji Ansilla kwa msaada mkubwa sana katika maish yake, na alisema anakumbuka birthday yake Nabii Flora alifanyiwa na mchungaji huyu. Pia alimshukuru Octavian ambaye alikuwa akimsaidia sana katika kupiga picha wakati akihubiri kwa kutumia kamera yake na bila malipo, alimshukuru sana Mchungaji Komba kwani amekuwa bega kwa bega tangia wameanza huduma hii, alimshukukru Mchungaji Jury kwa kukubali kufanaya naye kazi ya Mungu kwani mara ya kwanza wamekutana Nabii Flora alimwambia ninaona una huduma ya uchungaji ndani yako lakini Mchungaji Jury hakutambua hilo na sasa ni Mchungaji katika kanisa la Nabii Flora. Aliwashukuru wazee wa kanisa kwa kazi wanafanya katika nyumba ya Mungu. Alimshukuru sana katibu wa kanisa kwa wametoka naye mbali sana katika kazi ya Mungu. Alimshukuru sana sana Salma ambaye ni mtu wa kwanza kufanya naye kazi ya Mungu, Salma alikuwa akimsaidia Nabii Flora kumpeleka saloon, kumsafirisha kipindi hana gari, kumtia moyo asonge mbele na mambo mengi mengi sana.


Kikundi cha vijana kikielekea madbahuni kwaajili ya kufungua Shampeni




 Wakiwa wamevua kofia kwa kumheshimu Nabii Flora baada ya kufika madhabahuni kwa zoezi la kufungu shampeni
 Kilifika kipindi cha kucheza na kufurahi
 
Nabii Flora akifanya Maombezi kwa kufungua shughuli ya leo
Wakisujudu wakati Nabii Flora akifanya maombi

Nabii Flora katika maombi


 Nasbii Flora akisubiria nini kinafuata baada ya maombi
 Mmoja wa watumishi wa Mungu akimpa glasi kwajili ya shampeni
 Watumishi wa Mungu wakifungua Shampeni







VIJANA WASHEREHEKEA SABA SABA HOSPITALI YA AMANA KUTOA MISAADA NA MAOMBI


Kundi la vijana kutoka kanisa la Living water Kitunda jijini Dar es salaam, hapo jana walisherehekea sikukuu ya sabasaba kwakwenda kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Amana iliyopo wilayani Ilala jijini Dar es salaam kwakuwapa misaada mbalimbali pamoja na kuwafanyia maombi.

Katika mahojiano na GK mtumishi Gasper Madumla kutoka knisa hilo ameelezea vitu mbalimbali walivyotoa kwa wagonjwa na hali ilivyokuwa "Tulienda Amana hospital kwa ajili ya maombezi na misaada kwa wagonjwa hususani hodi ya wazazi. tulipangiwa wodi ya wazazi kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni. tuliwapelekea vitu kama dawa za matibabu,Vifaa tiba mfano nyembe,groves,tishu,sindano,pamba,pia sabuni,pia tulifanya maombi kwa wakina mama waliojifungua na hata wale waliokuwa hawana uchungu nao wote wakapokea uponyaji mkuu.Pia tulikuwa na vifaa tiba vingine kama Derto,pempasi, Tulianza kwa kufunga na kuomba wiki nzima kabla ya kwenda hospitalin ili msaada huo uwe na uponyaji ndani yake niliendesha maombi ya nguvu kabla tu hatujafika hospitali kwa kuvitakasa vifaa hivyo kwa yeyote yule mwenye kuvitumia vimponye bila kujali dini au itikadi yake ya dhehebu" amesema mtumishi Madumla

Aidha mtumishi huyo ameongeza kuwa"Na baada tu ya kuwasili hospitalini hapo,tulipokelewa vizuri sana kisha tukaoneshwa wordi ya wazazi mahali ambapo wakina mama mara nyingi wajifunguapo hupoteza watoto wao,au mara nyingi hujifungua kwa taabu sana,hivyo tulipopelekwa katika wordi hiyo,tukaanza kazi ya kuwapa misaada na kufanya maombezi rasmi ili isije ikajitokeza hali ya kupoteza mtoto na hata uchungu uwe wa kawaida kwamba Bwana afanye wepesi katika hali yao ya kujifungua. Kwa sababu ilikuwa ni wordi ya wazazi,walipendelea waingie wanawake kwa huduma ya kiroho maana nilikuja nao wanawake ambao ni watumishi wa Mungu,nao wakaichapa kazi vizuri ,hakika wote walibarikiwa. Ilipofika saa kumi na mbili tulikuwa tumemaliza na kuanza kurejea nyumbani.




 Source: GK
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...