HEADER

Jumanne, 11 Juni 2013

WORSHIP HOUSE WAOMBA KURA KWA WATANZANIA, TUZO ZA INJILI AFRIKA


Kundi la Worship House kutoka jimbo la Limpopo nchini Afrika ya kusini limewaomba Watanzania kuwapigia kura ila waweze kuibuka na tuzo ya kundi bora la mwaka, tuzo ambayo wanawania na makundi mengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Akizungumza na GK mmoja wa viongozi wa katika kanisa la Christ Worship House linakotokea kundi hilo bwana Khathu Makhuvha, ameiomba GK kulifikisha hili kwa wapenzi wa muziki wa gospel nchini watakapokuwa wakiwapigia kura waimbaji wao(wetu) Christina Shusho pamoja na Martha Mwaipaja basi wasisahau kuwapigia kura Worship House kupitia kipengele cha Group of Year ambapo jina lao lipo humo, pia watafanya hivyo kwa waimbaji wetu.

Worship House limepata tuzo mbalimbali nchini Afrika ya kusini, pia WAPO radio imekuwa ikipiga nyimbo zake mbalimbali kutoka toleo la tatu na la saba. Kama hujapiga kura ni wakati wako sasa wapigie kura waimbaji wetu ambao wanatuwakilisha kupitia kipengele cha mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki "Artiste of the year East Africa" ambapo utaona jina la Martha Mwaipaja pamoja na Christina Shusho mpigie kura mmoja wao kisha usiwasahau na Worship House. kumbuka mwisho wa kupiga kura yako ni tarehe 30 June 2013. Namna ya kupiga fuata maelekezo hapo chini

1 Click hapa Africa Music Gospel Awards

2. Kisha Bonyeza Kitufe Chenye neno "Vote".

3. Utaingiza Email address yako.

4. Kisha utafuata maelekezo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...