HEADER

Jumatatu, 3 Juni 2013

NABII FLORA: MAHUBIRI YA TAREHE 29.05.2013. SOMO NA UTABARIKIWA NA MAHUBIRI HAYA

Mwandishi: Rumafrica

Nabii Flora Peter
Atakulinda Yeye wala hata sinzia, hata kubali mguu wako usogezwe wachawi wasogeze mguu wako, kifo kisogeze mguu wako, mateso yasogeze mguu wako yaani hata kubali atakulinda pokea, anaema sinta kuacha jua halite kupiga mchana wala usiku. Nataka ulindwe mama nyumba yako izungushiwe kuta za moto wanapotuma vingwendu, roboti zitashindwa kufanya kazi.

Mchungaji Komba
Naona mamlaka zinatembea anasema duniani ni sehemu yangu ya kuweka mguu wangu, naona miguu ya Yesu inatembea inakausha Ukimwi, Kansa, uvimbe, inaondoa magonjwa, utasa, mapepo inamamlaka ikikanyaga inafuta mateso. Nasema na watu wanaonitazama kwenye youtube maana upo mguu yapo mamlaka ya Yesu yameshuka leo.
Anasema duniani ni sehemu yangu ya kukanyaga lakini mbinguni ni sehemu ya kiti change cha enzi, nataka Bwana asimame leo, naona mamlaka inatembea naona uweza wa Yesu naona miguu ya Yesu mama anakanyaga magonjwa, umasikini, Ukimwi, mapepo, utasa, mateso chini ya kitovu nakwambia achia utaweka mamlaka ya Yesu. Unamaruhani , unamizimu, unamajini mahaba ipo mamlaka inakanyaga, sauti ya Yesu inakuita fanya hima ufike haraka anakuita wewe unayenitazama kwenye yuotube, unayenisoma kwenye facebook na blogu sauti ya Bwana inakuita asubuhi ya leo.
Anakuita wewe muombaji ulikuwa unaweza kuomba lakini sasa hivi unapiga miayo tu sauti ya Bwana inakuita baba, mama, kijana usifanye moyo wako kuwa mgumu sauti ya Bwana inakuita ameshuka mwenye mamlaka ipo sauti ya Mungu inawaita watanzania, watu mbalimbai wanaonitazama kwenye youtube na kunisoma kwenye blogu na facebook yupo Yesu anakuita leo.
 Anasema geuke unapokwenda unaenda kuangamia hiyo biashara waliyo kushirikisha nakwambia sio sahihi unakwenda kukamatwa utaishia sero nakwambia acha biashara hiyo wewe unayenitazama kwenye youtube, unayeshirikishwa biashara na rafiki zako wa tatu mmoja mfupi mweusi anamwanya chini mwingine mrefu amenyoa panki tena mweupe nasema hiyo biashara waliyo kushirikisha unakwenda kukamatwa utaishia polisi. Usikiapo sauti hii nasema geuka ipo Baraka zipo kazi nyingi nyingi mbele za Bwana utafanya kazi zako utabarikiwa.

Hakika ninasika sauti ya Bwana inakuita, Mtanzania , mwana Dar es salaam kwamba njoo uitende kazi yake wewe unayekaa vijiweni hasubuhi mpaka jioni wewe unafuata tu kivuli sauti ya Yesu inakuita leo, inakuita uje utende kazi yake.

Usikiapo sauti hii geuka wakati wa neema ni sasa usije ukakawia ukachelewa ukakuta neema kwako imeondolewa, Yesu anakuita asubuhi ya leo amesema duniani ni sehemu ya kuweka miguu yake mbinguni ni nsehemu ya kiti chake cha enzi. Anataka akanyage mateso kwako maana ipo mamlaka kwake akikanyaga anaondoa taabu zako zote.
Somo linatoka katika kitabu cha Mwanzo 28:16-22
Mwanzo 28:16-22
Nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa Baba yangu ndipo na wewe Mungu utakapo kuwa Mungu wangu. Na jiwe hili ninalo lisimamisha hapa nitaijenga nyumba yako Bwana, na kwa kila kitu kitakapopita mikononi mwangu nitakutolea wewe Mungu. Yakobo alipoamka asubuhi na mapema akalitwaa lilie jiwe alilokuwa ameliweka juu ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake akapaita mahali pale jina lake Betheli, lakini ule mti baada ya hapo ulikuwa unaitwa Luzu. Yaani Luzu ni mji wenye ukame
Mchungaji Komba akitafsiri lugha ambayo nabii Flora alikuwa akinena
Yamkini wewe unaitwa mtu ambaye awezi kuwa na gari, nazungumza na mtu ambaye leo anahitaji kubadilika, wewe unayetaka kubadilika kutoka katika hali ya ukame na huitwe mtu mwenye Baraka, uliye nawiri. Maisha yako yabadilike ulikuwa unakunywa chai ya rangi unywe chai ya maziwa, ulikuwa unakula mlo mmoja ule milo mi tatu utatoka katika hali ya kuitwa Luzu na utaitwa Betheli.
Bwana akamwambia msipande mazao katika mji wa Luzu, mji wa Luzu ni mji wenye jiwe la chumvi hauoteshi chochote. Kwa hiyo sasa naamuru watu hawa wasipande chochote katika mji wa Luzu; yaani mti wa Luzu unajikutaumetoa sana sadaka huoni kinachoendelea ni mji wa Luzu umepanda, umetoa fungu la kumi lakini bado umefilisika, ulitoa Luzu sasa njoo weka hapa Betheli. Yaani jiwe la chumvi hauoteshi chochote hata maji ukiyanywa hayana ladha.

Dada kichaa aliyeletwa kwa maombezi
Nendeni Betheli mkapande kila aina yam mea na kila aina ya nafaka na kila mti wa matunda, pandeni humo katika mji wa Betheli kwa sababu udongo wake, udong wa baraka. Hii ni huduma ya Baraka hata kama umeachwa na mume, mume atwrudi kwa mke wake  wan ndoa panda miguuni kwa Nabii maana kuna udogo mzuri. Yaani katika kanisa la Yesu ipo miujiza watu wanapona Ukimwi, vipofu wanaona, viwete wananyooka miguu, vilema wanafunguka panda hapa katika mji wa Betheli, umekataliwa hujazaa umetolewa kizazi panda mbegu zako hapa hakika utazivuna.
Yakobo akaamka katika usingizi wake akasema  kweli bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua kama bwana  yupo. Naye akaogopa akasema kweli Mungu yupo mahali hapa wala mimi sikujua,  na hapa ndipo lango loa mbinguni. Yamkini wewe umekuja Mtanzania, unayenitazama kwenye youtube, unayenisoma kwenye blogu na facebook. Yakobo alishangaa akasema mbona  hapa panatisha kama nini akasema bilashaka hapa ni nyumba ya Mungu, miujiza watu wanapona magonjwa mbali mbali, akisema hewa geuka inageuka, akisema miti sujudu miti inasujudu maana hapa panatisha kama nini.
Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe lililokuwa chini ya kichwa chake akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake akapaita mahali pale jina lake Betheli. Nami nakutamkia Baraka siku ya leo ya kureje fedha na shekel, nakutamkia Baraka hata kama ulitamkia laana na mama mkwe, mama yako, shangazi naifuta laana nakutamkia baraka.
Yakobo akaweka nadhiri akasema Mungu ikiwa atakuwa pamoja nami, akinilinda katika safari ninayo iyendea na kunipa chakula nile, na mavazi nikavaa na nitarudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu na jiwe hili ninalo lisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu hapa, na katika kila utakalo nipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Laana zilimpata baba yetu wa imani ndipo watoto wake wa kwanza wa kiume walilala na wake zake, ukitoa nadhiri usipo hiyondoa na ndo maana mimi nilimwambia Mungu kama utanifanikisha nimalize jengo Salasala nitakutolea ng’ombe ili watoto wangu wasije wakafanya laana wao kwa wao. Ili laana niifute nilichinja ng’ombe wa  tatu, watu hawakujua nilitoa nadhiri kwa Mungu nikamwambia Mungu kama utanifanikisha nikalimaliza jengo hili kwa miezi mi tatu nitakutolea ng’ombe.
Kumbe nadhiri ni kitu sio cha mchezo ukisema Nabii nitatoa fungu la kumi toa, chagueni sasa leo kama utakuwa Luzu ama utakuwa Betheli. Yaani Luzu ni nchi isiyo kubali zao lolote, chakueni wa baba na wa mama  unapenda kukaa nchi gani na leo ni siku ya tatu ya uumbaji ambayo Mungu aliumba, Mungu nataka  leo uwatendee watu hawa.

SIKILIZA USHUHUDA WA KIZITO
Kwa jina naitwa Kizito nilikua hapa nikiwa na matatizo yangu ma nne nikaa na Nabii nikamweleza matatizo yangu, akasema nichague tatizo langu moja ili niweze kuliombea basi nikamwambia naomba kazi. Nilikuwa naimesha tumia juhudi zngu za mwili na elimu yangu lakini haikuwezekana, nilikuwa nimeshapeleka application za kazi karibu hamsini lakini sikujibiwa hata moja. Baada ya kuja hapa Nabii akaniambia naona ukuta mkubwa sana juu yako na sasa naingia kwenye maombi kuuvunja huu ukuta, na kweli siku ambayo alikuwa ameniahidi nitapata kazi, siku moja kabla nikapokea email kwamba nipo tayari kufanya kazi. Na siku ambayo Nabii aliniambia ndiyo nitapata kazi nilipigiwa simu niende nikafanye interview, kwa kweli hapa mmefika ndo mahali pake.
Yakobo akaweka nadhiri akasema Mungu ikiwa atakuwa pamoja nami, akinilinda katika safari ninayo iyendea na kunipa chakula nile, na mavazi nikavaa na nitarudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu na jiwe hili ninalo lisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu hapa, na katika kila utakalo nipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Tutakuwa na wageni mbali mbali siku ya jumapili  watatembelea katika kituo hiki, kutakuwa na ibada ya ajabu sana kwa kweli ni ya kuufungua mwezi na nikwambie mwezi huu unalenga nini na nikwambie haki zako za mwezi wa sita. Nataka nikwambie leo ni tarehe 29 tunaelekea kufunga mwezi Abuu, kesho tarehe 30 tunamalizia Ijumaa, Jumamosi tarehe 1 na Jumapili itakuwa tarehe 2, itakuwa ni ibadayetu ya mwanzo wa mwezi ambayo tutapaka mafuta.
 Kila ilipofika mwisho wa mwezi Nabii Eliya alipita kwa mwanamke mshumemo, ataalipokuwa mapambavuko aliingia katika ile nyumba ya mwana mke wa cheo, nitakupa habari za mwana mke mshumemo walipokuwa wakiingia nyumbani kwa mtumishi wa Mungu alipanda kitu gani. Mwanzo wa mwezi, mwisho wa mwezi ni kitu gani kinatokea.
Ujapozimwa nyota hapa inang’aa, hata kama wameizima wameikalia, wameifunika hapa tunaifungua kwa jina la yesu.
SHUHUDA
DADA ALIYEKUWA ANATAFUTA  KAZI  SASA  AMEPATA
Bwana Yesu asifiwe, kwa jina naitwa Mwajabu; asubuhi mimi nilikuja nikamwambia Nabii kwa nini mimi sipati kazi, Nabii akaniombea akaniambia kuanzia sasa hivi naamuru upate kazi, narudi kukaa kwenye kiti napigiwa  simu naambiwa kunakazi kwenye sekondari moja ambayo nili applay nimeambiwa  nikaanze kazi.
KIJANA ALIYEKUWA AMEPOTEA SASA AMERUDI NYUMBANI
 Pia nilikuja hapa na mama mwenye nyumba wangu akamwambia Nabii kijana wake amepotea Nabii akamwambia ataonekana kweli  baada ya maombi siku hiyo tupo sokoni na dada yake tukamuona, ndo akarudi nyumbani moja kwa  moja.
DADA ALIYEKUWA ANAOMA KALI SASA AMEPOA
Kwa jina naitwa Beatrice Wiliamu; mimi namshukuru Mungu wa  madhabahu hii ameniponya, ni juzi tu nilkuwa naumwa sana yaa kiukweli hali yangu ilikuwa mbaya mno kichwa kinauma homa kali natetemeka. Sasa wakati naumwa  na mbwa wangu na yeye alikuwa anaumwa sana, basi mdogo wangu akampigia Nabii akamwambia aniombee, baada ya Nabii kuniombea nikajisikia nafuu lakini baada ya kuamka asubuhi nikajikua mzima, yaani ile vita ilikuwa ni kubwa mbwa wangu yeye alikufa.
MTOTO ALIYEKUNYWA SUMU AMEPONA
Kwa jina naitwa Anastanzia Elius; nashukuru madhabahu ya Nabii Flora yanazidi kuniokoa tu maana kila niachohitaji  nikija hapa nikiomba Mungu ananitendea. Mimi juzi nilipigiwa simu nikaambiwa mdogo wangu anaumwa sana aikuwa amekunywa sumu, lakini baada ya maombi amepona kwa kweli namshukuru Mungu.
MAMA ALIYEKUWA NA UGOMVI NYUMBANI KWAKE SASA MAELEWANO YAMERUDI
Kwa jina naitwa Johanitha; mimi nimeanza maombi hapa mwezi wa pili, nilikuwa ninavita kwenye familia yangu mpaka nafika hatua nakata tama, lakini baada ya maombi namshukuru Mungu amenirudishia amani ndani ya nyumba yangu, mume wangu amerudi na mgogoro na mama mkwe wangu umeisha namshukuru sana Mungu.
MTOTO ALIYEKUWA ANAUMWA SASA AMEPONA
Kwa jina naitwa Leah;  mimi namshukuru Mungu kupitia madhabahu hii kwa sababu wiki iliyopita mtoto wangu alikuwa naumwa sana, nimempeleka Hospitali  lakini bado amepimwa hana ugonjwa, nikampeleka tena Hospitali nyingine ndo akakutwa na almonia. Lakini mishipa ikawa haionekani, nikampigia Nabii simu akamumbea mishipa ikaonekana na akapatiwa huduma, nmshukuru Mungu mwanangu amepona mpaka  leo.




 Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji Mbezi Salasala Dar es Salaam Tanzania
Tembelea: www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com
Mob: +255 657442699   


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...