HEADER

Jumanne, 11 Juni 2013

KUMEKUCHA, MTU MWINGINE AJITAMBULISHA KWAMBA NI YESU AFRIKA KUSINI



Moses Hlongwane aliyejitangaza kwamba ni Yesu nchini Afrika ya kusini. (Photo: eNCA video Screencap)

Ikiwa takribani wiki moja na siku kadhaa kupita tangu mtu mmoja aitwaye Alan John Miller kutoka nchini Australia kujitangaza kwamba yeye ni Yesu huku mkewe akimtambulisha kwamba ndiye Maria Magdalena, huko nako nchini Afrika kusini mtu mwingine mzawa wa nchini humo aitwaye Moses Hlongwane anajitangaza kwamba yeye ni Yesu na tayari amepata mamia ya wafuasi ambao wamekuwa wakichanga pesa ili kuhakikisha ujumbe wake unaenea duniani.

Bwana Moses Hlongwane mkazi wa KwaZulu-Natal amekuwa akitumia muda mwingi nyikani kama ilivyokuwa Yesu alivyomshinda shetani na kuonyesha kwamba yeye ni mwana wa Mungu

" Nimekuwa ndani ya chumba hiki toka mwaka 1992 nimetumia miaka 22 nikipambana na shetani na nimemshinda" amekaririwa mkazi huyo wa Afrika ya kusini Aidha ameendelea zaidi katika kuzungumza kwake kwa kusema "Hata sasa ninavyozungumza sitakufa tena, nasasa najiandaa kufungua makaburi, kuponya vipofu na walemavu" huyo ni Moses Hlongwane au Yesu kama alivyojitambulisha mwenyewe katika mahojiano na kituo cha eNews nchini Afrika kusini.

Aidha kituo hicho kimemfanyia mahojiano mmoja wa wafuasi wa bwana Hlongwane aitwaye Paul Sibiya(84) ambaye ameamua kutoa kiinua mgongo chake chote kwa mtu huyo anayeamini kwamba ni mwana wa Mungu" Mimi naishi kwa kiinua mgongo, ruzuku(pension) lakini huwa situmii ruzuku yangu kumsaidia mke wangu bali natoa kwa mfalme wa wafalme ambaye ndiye anainua kipato changu", amekaririwa Sibiya.

Mke wa mfuasi huyo aitwaye Alfin amesema mumewe anaamini kwakufanya hivyo anatoa moyo wake kama sadaka. Baadhi ya wanafunzi wake na bwana Hlongwane wapo ambao wana umri wa miaka 14 ambao nia yao ni kuhakikisha wanapeleka ujumbe duniani kwamba Hlongwane ndiye Yesu Kristo.

Bwana Alan (50) wa Australia ambaye ni mstaafu wa mambo ya Komputa aliyejitangaza kwamba yeye ni Yesu amekaririwa kwenye tovuti yake akisema kwamba walikuja duniani mara ya kwanza zaidi ya miaka 2000 iliyopita, jina lake likiwa Yeshua mwana wa Yusufu au Yesu wa kwenye Biblia, mtoto wa Mariam na Yusufu. Kisha Mariam Magdala ambaye kwenye Biblia maetambulishwa kama Mariam Magdalena ambaye ndiye mke wangu na ndiye mtu wa kwanza niliyemtokea baada ya kufufuka, ndivyo alivyoandika katika tovuti yake pamoja na dvd zake zikionyesha akijibu maswali mbalimbali.


Kwa upande wa mchungaji Dkt. David Millikan wa kanisa la Uniting Church Theologian, ameonya kuhusu yanayotokea sasa kwamba yataleta madhara kwa wafuasi wa watu hao, kwakuwa kutokana na hayo wanayoyasikia wataendelea kuvutwa karibu zaidi na kushindwa kufanya mambo mengine ya maendeleo yako binafsi kwakuwa utatumia pesa zote, utakuwa na matatizo ya mawasiliano na familia yako ambayo yatasababisha mahusiano kuvunjika, amesema mchungaji huyo

Watu mbalimbali ambao wamezungumzia habari za watu hao kila mmoja amekuwa akinukuu mstari kutoka kitabu cha Mathayo 24:5 unaozungumzia manabii wa uongo kila mmoja akijiita yeye ni Kristo na kudanganya wengi.

ChristianPost
Source: GK

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...