HEADER

Ijumaa, 14 Juni 2013

KURA ZIMWAGIKE KWA WATANZANIA JUU YA TUZO ZA MUZIKI WA INJILI TANZANIA

Kama ilivyokawaida Miaka iliyopita tumekuwa tukitoa Mwakilishi katika Tuzo za Muziki wa Injili Afrika (AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS) hasa katika kipengele cha Mwimbaji Bora wa Mwaka Afrika Mashariki.

Mwaka huu 2013, tumefanikiwa kuwa na Wawakilishi wawili katika Category Moja, ambao ni Christina Shusho na Martha Mwaipaja. Mwaka jana Christina Shusho alituwakilisha Watanzania ingawa hakuweza Kushinda tuzo hiyo kutokana na Uchache wa Kura.

Sasa hebu Mwaka huu tuhakikishe Ushindi unarudi Tanzania. Kama bado hujapiga kura basi ni wakati wako sasa. Wapigie kura waimbaji wetu toka Tanzania, ambao wanatuwakilisha kupitia kipengele cha Mwimbaji wa Mwaka Afrika Mashariki "Artiste of the year East Africa" ambapo utaona Jina la Martha Mwaipaja na Christina Shusho. Mpigie kura mmoja kati ya hawa wawili.

Namna ya kupiga kura fuata maelekezo yafuatayo;

1 Tembelea: www.africagospelawards.com

2. Kisha Bofya sehemu iliyoandikwa "2013 NOMINEES AND VOTING".

3. Halafu Bonyeza Kitufe Chenye neno "VOTE NOW" (Mwisho kabisa wa Majina Yote).

4. Utaingiza Email address yako.

5. Kisha fuata maelekezo.

ZINGATIA: Uwe na "email address" inayofanya kazi, Na Mwisho wa Kupiga Kura ni June 30, 2013.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...