
Usimuone
mtu ana nguvu za Mungu ndani yake.. ana upako wa hali ya juu..
ukafikiri aliamka tu asubuhi na kujikuta hivyo... kuna gharama
amelipa... "wakati wewe unakula na kunywa, mwenzio alikuwa anafunga na
kuomba, wakati wewe unajikweza.. yeye alijinyenyekesha, wakati wewe
unafanya mambo yasiyo na faida kujifurahisha, yeye alikuwa anasoma neno
la Mungu na kutembea katika utakatifu, wakati wewe uko busy kuangalia
makosa ya watu ili uwakosoe, yeye alikuwa busy kujiangalia ni wapi
alipokosea na kujirekebisha, wakati wewe unakesha kwenye starehe, yeye
alikesha kwa kuomba nk.." Kwahiyo, chunga sana mdomo wako...!
You might also like:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni