HEADER

Ijumaa, 7 Juni 2013

MKONGWE WA MUZIKI DONNIE McCLURKIN AMKUBALI MWIMBAJI WA JOYOUS

Mwanadada aliyemaliza mkataba wake na kundi la Joyous Celebration la Afrika ya kusini, Mahalia Buchanan wiki iliyopita alitajwa kama mtu mwenye bahati baada ya kupewa nafasi ya kuimba na mkongwe wa muziki wa injili duniani Pastor Donnie McClurkin ambaye alikuwa nchini Afrika ya kusini sambamba na mwanadada nyota Cece Winans kwenye tour yao ya kimuziki nchini humo.


Pastor Donnie McClurkin na Cece Winans katika pozi. Picha ASSOCIATED PRESS-ROBERT GALBRAITH-Newscom-RTR

Mahalia ambaye alikuwa mwitikiaji katika shoo iliyofanyika kanisa la Grace Bible lililopo Soweto alipewa nafasi ya kuimba na mkongwe huyo wimbo wa "Great is your mercy" ambapo mwanadada huyo aliutendea kazi na kuinua kelele za shangwe kanisani hapo, kisha mkongwe huyo akamalizia kwakuwaambia umati wa watu uliohudhuria kwamba "Mahalia amemaliza kila kitu, mnatakiwa mkubali dhahabu hii mliyonayo" akionyesha kwa Mahalia.

Mahalia Buchanan
Mwimbaji huyo mkongwe pamoja na Cece waliweza kuwabariki wengi kwa uimbaji wao ambao uliwavuta watu waliohudhuria kwenye maonyesho yao karibu na Mungu wao, huku mwanadada Mahalia ambaye alikuwa ndio kwanza karejea kutoka Detroit nchini Marekani alikokuwa, akimshukuru Mungu pamoja na watu wanaompa sapoti katika huduma yake.

Thanks GK

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...