HEADER

Alhamisi, 13 Juni 2013

RULEA SANGA KATIKA IBADA YA LEO MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA

Ninamshukuru sana Mungu wangu wa huruma kwa kazi yake na upendo wake juu ya maisha yangu. Mungu amekuwa mwema sana kila kuitwapo leo. Ninajihisi kama nina wazazi wangu bado duniani hata kama waliniacha na kubatizwa jina lingine la YATIMA. Nimekuwa nikifarijika sana na Mtumishi wa Mungu Nabii Flora na Nabii TB Joshua kwa yale wanafanya juu ya maisha yangu. Mungu amekuwa mwema sana kwa kunipa kibali mbele ya watumishi hawa wa Mungu. Nabii Flora amekuwa kama marehemu mama yangu hapa duniani na Nabii TB Joshua amekuwa kama baba yangu ambaye sijawahi kumuona tangia nizaliwe na hata kuona kaburi lake mpaka umri huu. Waumini wa kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji wamekuwa kama kaka zangu na dada zangu kwani hapa mjini Dar es Salaama sina dada wala kaka kutoka katika familia ya Lanzon Sanga. Nimekuwa nikipitia mengi ya kukatishwa tamaa lakini Mungu kwa kupitia watumishi hawa amekuwa akinivusha na kunipa faraja.


Ninabarikiwa sana na huduma za Nabii na Mtume  Josephate Mwingira kwa maana amekuwa msaada wangu na kunilea katika kanisa lake la Efatha kipindi nimevunjwa moyo na watumishi wa Mungu na kutamkiwa maneno magumu sana kipindi mama yangu amefariki, nikiwa na wiki moja tu tangia nimzike mama yangu Uyole mjini Mbeya.

Ninawapongeza sana wa Glorious Celebration na Glorious Worship Team kwa kipindi nipo nanyi kihuduma, kwani nimefarijika sana na uimbaji wenu na huduma yenu kwa ujumla. Mungu azidi kuwa nanyi maisha yenu yote. Mungu abariki maisha yenu na muwe na mafanikio makubwa sana kihuduma na maisha ya kila mmoja.

Nabii Flora nitazidi kuwa nawe kwani umekuwa msaada mkubwa sana katika maisha yangu. Ninapoiona huduma yako natamani Mungu angeshuka na kukugusa ili watu waone na waamini kwa yale unafanya kwa wanadamu hapa duniani.

Siku ya leo umenibariki sana mtumishi wa Mungu Nabii Flora, na ilikuwa ni siku yangu ya pili kuhudhuria ibada za katikati ya wiki. Mungu ameonekana kwangu siku ya leo..kabisaaaaa.

Wewe ambaye hujawahi kufika kwa nabii Flora jitahidi ufike na ukifika wewe kaa pembeni na uone matendo makuu kwa kupitia mtumishi wa Mungu nabii Flora Peter.

Mimi nisikuchoshe ila ninaomba tushirikane kuona jinsi mkinga mimi nilipokuwa kanisani kwa nabii Flora siku ya leo Alhamisi.

Hapa nikiwa nimefika kanisani na kukaa viti vya nyuma kabisa.

Hapa nikiwa nimeitwa na nabii Flora na kuniambia sistahili kukaa viti vya nyuma..nikae na wazee wa kanisani. Kushoto kwangu ni mtumishi wa Mungu Mchungaji Ansila

Hapa nikitafakari Neno la Mungu la kwamba.."Ukijishusha utainuliwa" ni baada ya kukaa na wakuu. Mungu wetu ni waajabu sana.

kiukweli nilijisikia mtu mwenye amani sana, na kuona kuwa watu wengine waweza kukuona unathamani na wengine wakakuona huna thamani na kukulaani.

Nikiwa katika maombi makali huku nikimshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kuwa na wakuu wa kanisa hili.

Nabii Flora aliweza kuniita na kuniambia nimpakate huyu mtoto ambaye anaushuhuda wake wa ajabu sana (Tembelea www.nabiiflora.blogspot.com na katika facebook: Nabii Flora Peter..Utapata kujua juu ya mtoto huyu.

Nabii Flora akiwa na mtoto ambaye anaushuhuda wake mkubwa sana. Baada ya ahap aliniita na kunipa kazi ya kumpakata.

Mimi sijui labda ni maono ya mimi kuwa na mtoto mzuri kama huyu..Hahahaha sijajua!!





Nabii Flora aliweza kuteta mambo mawili katika ofisi yake ya kusikiliza matatizo ya mtu mmoja mmoja.

Hapa siwezi sema ila kuna jambo la kimsingi lilifanyika na hii ni kati yangu na Mungu wangu, ila jua tu Nabii Flora aliweza kuzungumza na mimi jambo la msingi sana  katika picha hii...

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...